About the portal
Kuhusu Mfumo
Niambie Resource Centre (Niambie’ is a swahili word meaning ‘Tell me’) is run by Benjamin Mkapa Foundation (BMF) with an aim of analyzing and sharing national status on HRH and service delivery specific indicators including HIV/AIDS and RMNCH as per national released reports and other program implementation reports and updates to the key stakeholders for evidence-based decision making toward improved access, quality and coverage of health services. Niambie resource Centre was developed as part of COMPASS Africa and funded by AVAC.
Niambie Resource Centre inaendeshwa na Taasisi ya Benjamin Mkapa ikiwa na lengo la kuchambua na kushirikisha utendaji kazi wa watumishi wa afya kitaifa kulingana na ripoti mbali mbali za kitaifa na za miradi katika viashiria maalum vya utoaji huduma za afya ikiwa ni pamoja na huduma za VVU/UKIMWI na Afya Uzazi, mama na mtoto kama ushahidi wa utoaji maamuzi kwa wadau mbalimbali ili kuimarisha upatikanaji, ubora na ufikiaji wa watu wote katika huduma za afya. Mfumo huu umetengenezwa kama sehemu ya shughuli za COMPASS, na umefadhiliwa na AVAC.
Who we are?
Sisi ni nani?
The Benjamin W. Mkapa Foundation (BMF), is a Tanzanian registered organization continues to work through partnerships in ensuring the health and well-being of the community, within Tanzania and the rest of Africa. BMF designs and rolls out different sustainable, innovative and cost-effective initiatives in health including HIV/AIDS, through advocacy, policy dialogues, operational research and implementation of interventions at community and local government authorities.
Taasisi ya Benjamin W. Mkapa ni shirika lililosajiliwa Tanzania, linafanya kazi kwa ushirikiano na wadau mbalimbali katika kuhakikisha afya na ustawi wa jamii, ndani ya Tanzania na Africa nzima. BMF hubuni na kuendeleza mipango mbalimbali yenye gharama nafuu katika masuala ya afya ikiwemo VVU/UKIMWI kupitia uraghabishi wa mijadala ya sera, tafiti mbalimbali na utekelezaji wa shughuli mbalimbali katika jamii na serikali za mitaa.
How we work
Tunafanyaje Kazi
We process data from various government and collaborating development partners reports and makes updates on specific HRH agendas and other service delivery indicators in a user friendly modular. Multiple updates are performed by our technical team who validate data from different reports and official announcement made by responsible authorities from the national to Global level.
Tunachambua taarifa kutoka kwenye ripoti mbali mbali za serikali, washirika wa maendeleo na kuhuisha (update) taarifa juu ya ajenda maalum za rasilimali watu katika sekta ya afya na viashiria vingine vya utoaji wa huduma kwa njia rahisi na rafiki. Taarifa zinazohuishwa hufanywa na timu yetu ya kiufundi inayothibitisha taarifa kutoka kwenye ripoti tofauti na matangazo rasmi yanayofanywa na mamlaka zinazohusika kutoka ngazi ya kitaifa hadi Ulimwenguni kote.
Sources and references
Vyanzo vya Taarifa
We process data from various government and collaborating development partners reports and makes updates on specific HRH agendas and other service delivery indicators in a user friendly modular. Multiple updates are performed by our technical team who validate data from different reports and official announcement made by responsible authorities from the national to Global level.The main reference sources are mainly from the Government reports obtained from Government Health Information systems, Official Websites of Ministries of Health or other Government Institutions, Health Sector National Platforms and Government Authorities’ Speeches. A technical team monitors reports released that among others, affect HRH matters. Sometimes, we use the trusted news sources reported by Governments and Non- government institutions in live press conferences before it is published on the Official Websites.
Vyanzo vikuu vya taarifa ni ripoti za serikali zinazopatikana kutoka kwa Mifumo ya taarifa ya afya ya serikali, tovuti ya wizara ya afya au taasisi zingine za serikali, sekta za afya, majukwaa ya Kitaifa na hotuba za kiserikali. Timu ya kiufundi inafuatilia ripoti mbalimbali zinazohusisha masuala ya rasilimali watu katika sekta ya afya. Mara nyingine tunatumia vyanzo vya habari vya kuaminika vilivyoripotiwa na serikali na taasisi zisizo za kiserikali katika mikutano ya moja kwa moja ya waandishi wa habari kabla ya kuchapishwa kwenye tovuti rasmi.
